Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchaguzi nchini Algeria ni fursa ya kushugulikia haki ya kukusanyika:Kiai

Uchaguzi nchini Algeria ni fursa ya kushugulikia haki ya kukusanyika:Kiai

Mjumbe maalum wa UM kuhusu haki za kukusanyika kwa amani Maina Kiai ametaka utawala nchini Algeria kutumia fursa ya uchaguzi wa ubunge unaokuja kuhakikisha mabadiliko yaliyofanywa kwenye mashirika ya umma ya mwaka uliopita yameafikia viwango vya kimataifa vya haki za binadamu.

Kiai amesema kuwa uchaguzi unaopangwa kufanyika tarehe kumi mwezi huu ni lazima uhakikishe kuw kuna haki ya kukusanyika. Amesema kuwa ni jambo la kujutia kuwa Algeria imepiga hatua nyuma kwenye masuala ya haki ya kusema na kukusanyika. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)