Wataalamu wa UM walaani hukumu kali zinazotolewa kwa watetesi wa haki za binadamu

4 Mei 2012

Kundi la wataalamu huru kutoka Umoja wa Mataifa wameshutumu kukamatawa na hukumu kali zinazotolewa kwa watetesi wa haki za binadamu nchini Iran na kutaka serikali ya nchi hiyo kuhakikisha kuwa watetesi wa haki za binadamu hawalengwi wakati wanapotekeleza wajibu wao.

Wataalamu hao wamezungumzia hali ya Nagress Mohammadi, makamu wa rais kwenye kituo cha watetesi wa haki za binadamu ambaye afya yake inatajwa kuwa mbaya na ambaye alikamtwa tena ili kuendelea na kifungo chake cha miaka sita. Wataalamu hao wametaka kuachiliwa mara moja kwa watetesi wa haki za binadamju na watu wengine waliokamatwa na kufungwa kwa kutetea haki za binadamu kwa amani nchini humo.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud