Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban aelezea wasiwasi wake nchini Guinea-Bissau

Ban aelezea wasiwasi wake nchini Guinea-Bissau

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa pamoja na kuwepo kwa ufuatiliaji wa karibu wa jumuiya za kimataifa, lakini hali jumla ya mambo nchini Guinea Bissau bina ni ya kusikitisha.

 Ban amesema utawala wa kijeshi umevuruga sura jumla ya taifa hilo huku mifumo ya kijamii, sekta za uchumi na mafungamano ya wananchi yakivurugwa vibaya.

Amesema matumaini ya wengi ni kuona kwamba nchi hiyo inarejea kwenye utengamao wake wa kawaida,huku katiba ya nchi hiyo ikipewa fursa yake.

 Ban amezungumzia umuhimu wa Umoja wa Afrika kwa kushrikiana na jumuiya ya maendeleo magharibi wa Afrika ECLOWAS kutafutia ufumbuzi wa haraka mkwamo huo ambao amesema unazorotesha ustawi wa taifa hilo.