Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwanadiplomasia wa UM aitaka Israel kuzingatia afya za wafungwa wa Kipalestina

Mwanadiplomasia wa UM aitaka Israel kuzingatia afya za wafungwa wa Kipalestina

Hali za afya za wafungwa kadhaa wa Kipalestina wanaoshikiliwa katika gereza moja huko Israel inaarifiwa zinazidi kuwa mbaya kutokana na mgomo wa kutokula wanaoneendelea nao wakipinga hatua ya kushikiliw akwao.

 Afisa mmoja wa Umoja wa Mataifa mbali ya kusikitikia hali za wafungwa hao, lakini ameitaka Israel kuchukua mkondo mpya kunusuru afya za wafungwa hao.

 Wafungwa hao wamesusia kula chakula chochote kwa kipindi cha miezi miwili sasa na afya zao zinazidi kuwa mbaya. Wangugwa wengine wapatao 1,000 walimaliza mgomo wa kutokula wiki mbili zilizopita.

Mratibu maalumu wa Umoja wa Mataifa katika eneo mashariki ya kati, Robert Serry,amezitaka pande zote kusaka ufumbuzi wa mapema kabla mambo hajaharibika zaidi.