Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kongamano la vijana la UM laangazia ajira kwa vijana

Kongamano la vijana la UM laangazia ajira kwa vijana

Karibu vijana milioni 81 wakiwa hawana ajira duniani Umoja wa Mataifa umeandaa kongamano kujaribu kutafuta suluhu la tatizo hilo. Idadi hiyo ilitolewa na shirika la kazi duniani ILO ambalo linasema kuwa tangu kuanza kwa hali mbaya ya uchumi duniani ukosefu wa jiara umekuwa ukiongezeka kote duniani.

Ronan Farrow ambaye ni mshauri wa waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani kuhusu masuala ya vijana duniani anasema kuwa kati ya hatua zinazostahili kuchukuliwa ni kuhakikisha elimu ni nafuu kwa minaji ya kuweza vijana kupata ajira.

(SAUTI YA RONAN FARROW)