Vyombo vya Habari bado vinakandamizwa nchini Burundi

11 Mei 2012

Wakati dunia imeadhimisha Siku ya Kimataifa ya Uhuru wa Vyombo vya Habari hivi karibuni, kwa taifa la maziwa makuu la Burundi, ilikuwa kama jinamizi. Nchini humo maadhimisho yalighubikwa na sauti kali za wanahabari ambao wanalalamikia utawala kutokana na kuzuiliwa gerezani kwa mwandishi wa habari wa Redio ya kibinfasi na ripota wa Redio ya Kimataifa Ya Ufaransa RFI Hassan Ruvakuki kwa tuhuma za kushirikiana na makundi ya wahalifu wa ugaidi.

Tukio hilo limewafanya wanahabari wengi kujiliza endapo uhuru wa vyombo vya habari una thamani yoyote kwa serikali ya taifa hilo. Wanahisi kushikiliwa kwa mwenzao kunatishia uhuru wa wanahabari lna pia kutia dowa baya kwa Burundi baada ya taifa hilo lilotoka vitani kusifika awali kutokana na vyombo vyake vya habari kuchangia kikamilifu katika mpango wa amani na maridhiano.

Kutoka Bujumbura, Muandishi wetu Ramadhani KIBUGA amefuatilia hali nzima ya uhuru wa vyomvo vya habari Burundi na kutuandalia makala haya . Ungana naye.

(FEATURE HABARI BURUNDI)

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter