Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNRWA yajutia mgomo wa vyama

UNRWA yajutia mgomo wa vyama

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi wa kipalestina UNRWA limeelezea kujutia kwake kufuatia mgomo unaoendekea likisema kuwa liko tayari kwa mazunguzmao kwa lengo la kupatikana kwa suluhu.

UNRWA inataka vyama husika kuachana na hatua kama hizo kwa kuwa zinawaathiri wakimbizi. UNRWA inatoa usaidizi na usalama na wakimbizi wa kipalestina nchini Jordan, Lebanon, Syria na eneo la kipalestina linalokaliwa na Israel. Shirika hilo linawahudumia karibu wakimbizi milioni tano kwenye masuala ya elimu ya msingi , huduma za afya na kuboresha kambi kwa ujumla.