Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM ina wasiwasi kuhusu hatma ya raia wa Sudan Kusini waliokwama Kosti

IOM ina wasiwasi kuhusu hatma ya raia wa Sudan Kusini waliokwama Kosti

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limeelezea wasi wasi uliopo kufuatia tangazo kutoka kwa gavana wa jimbo la White Nile kwamba mashirika ya kimataifa na raia wa Sudan Kusini wanaosubiri kusafirishwa kutoka eneo la Kosti wana hadi tarehe tano mwezi huu kuondoka. Kwa sasa kuna kati ya raia 12,000 na 15,000 kwenye eneo la Kosti lililo umbali wa kilomita 200 kutoka mji wa Khartoum ambapo wengi wao wamesubiri kwa miezi kadha kusafirishwa kwenda Sudan Kusini.

Makubaliano kati Sudan na Sudan Kusini ya tarehe 12 mwezi Februari yanaeleza kuwa kuhama kwa raia wa Sudan Kusini kwenda Kusini yatakuwa ni ya hiari na yanayofanyika kwa njia ya amani. Jumbe Omar Jumbe ni afisa wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE OMAR JUMBE)

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP linasema kuwa mapigano ya hivi majuzi kwenye eno la Kaskazni mwa mpaka wa Sudan Kusini huenda yakasababisha watu zaidi kukumbwa na njaa. Juma lililopita WFP iliwasaidia karibu wakimbizi 2000 kwenye jimbo la Unity na hadi sasa usamabazaji wa misaada unaendelea.