Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ofisi ya haki za binadamu ya UM yatiwa hofu na mauaji ya mwanaharakati wa mazingira Cambodia

Ofisi ya haki za binadamu ya UM yatiwa hofu na mauaji ya mwanaharakati wa mazingira Cambodia

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa mataifa leo imeelezea hofu yake kuhusu mauaji ya wiki iliyopita ya mwanaharakati wa mazingira, msema ukweli na mtetezezi wa haki za binadamu nchini Cambodia , mwanaharakati inayosema alikuwa akifanya kazi bila woga kuweka wazi shughuli haramu na ufisadi nchini humo.

Chut Wutty aliuuawa kwa kupigwa risasi Alhamisi iliyopita Kusini Magharibi mwa Cambodia kwa mujibu wa msemaji wa ofisi ya haki za binadamy ya Umoja wa Mataifa Rupert Colville, mwanachama wa Cambodian gendarmerie pia aliuawa katika tukio hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Colivelle amesema licha ya ukosefu wa taarifa za kutosha za nini hasa kilichotokea ofisi ya haki za binadamu inatiwa mashaka kwamba mauaji ya bwana Wutty yanadhihirisha mfululizo wa mashambulizi ya karibun ya kutumia silaha dhidi ya watetezi wa haki za binadamu nchini Cambodia.

Bwana Wutty aliuawa porini kwenye jimbo la Koh Kong na ofisi ya haki za binadamu mjini Phinom Pehn ilituma timu kwenye jimbo hil masaa mawili baada ya mauaji kuchunguza tukio hilo. Coliville amesema wnakaribisha hatua ya serikali kuanza uchunguzi ukiwemo wa kijeshi wa mauaji hayo.