Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maelfu ya watoto wako kwenye hatari ya kufa njaa Somalia

Maelfu ya watoto wako kwenye hatari ya kufa njaa Somalia

Shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF linasema kuwa zaidi ya watoto 325,000 wa Kisomalia ambao wanakumbwa na hali mbaya ya utapiamlo huenda wakafa miezi inayokuja kutokana na ukosefu wa ufadhili utakaowezesha watoto hao kuhudumiwa.

UNICEF inasema kuwa watoto hao bado wamesalia katika hali mbaya hata baada ya kuisha kwa njaa iliyoyakumba maeneo ya kusini na kati kati mwa Somali mwaka uliopita. Linasema kuwa bado familia nyingi zinakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula likiongeza kuwa hadi sasa limepokea dola milioni 30 tu kati ya milioni 289 lililoomba. Marixie Mercado kutoka UNICEF anasema kuwa huenda shirika hilo likasitisha mipango yenye lengo la kuokoa maisha kutokana na ukosefu wa fedha.

(SAUTI YA MARIXIE MERCADO)