Herbie Hancock kujitokeza kwenye tamasha la kwanza la Jazz

30 Aprili 2012

Balozi wa hisani wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na elimu, sayansi na utamaduni UNESCO Herbie Hancock amesema kuwa muziki wa jazz una utambulisho wa iana yake na hivyo kutohitaji tafsiri ya aina yoyote.

Mwanamuziki huyo mashuhuri ni miongomi wanamuziki kadhaa duniani wanaoshiriki tamasha lakwanza kimataifa la mziki wa jazz .

Tamasha hilo limeandaliwa na UNESCO likiwa na lengo la kuwaleta pamoja jamii ya watu mbalimbali ikiwemo wanahistoria, wanamziki, wasomi na watu wengine mashuhuri duniani.

Lengo kubwa la tamasha hilo ni kutoa funzo na utambuzi juu ya mziki wa jazz, huku pia likiangazia historia yake na hatma yake hapo baadaye.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter