Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zakir Hussain asema muziki wa Jazz ni ukombozi

Zakir Hussain asema muziki wa Jazz ni ukombozi

Wasanii kadhaa tayari wameanza kukusanyika kwenye ukumbi wa Baraza Kuu kujiandaa na onyesho la kimataifa na mziki wa jazz uliopangwa kufanyika April 30.

Ukumbi huo umeshuhudia vimbwanga vyote vinavyohusu mziki wa jazz huku wanamziki wanaotazamiwa wakifanya mazoezi ya mwisho mwisho na kurekebisha vifaa vyao.

Miongoni mwa wasanii wanaotazamiwa kutumbuhiza ni pamoja na Stevie Wonder, Sheila E, Jimmy Heath na Angelique Kidjo.Pia kwenye ukumbi huo anakutikana mwamuziki nguli Zakir Hussain.