Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban aitaka India kuboresha huduma za afya kwa wanawake na watoto

Ban aitaka India kuboresha huduma za afya kwa wanawake na watoto

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameitolea mwito India kuchukua nafasi ya usoni juu ya uboreshaji wa huduma za afya kwa makundi ya wanawake na watoto, akisisitiza kuwa kuleta ufumbuzi wa pamoja kwenye maeneo hayo ni hatua muhimu kwa mataifa ya kusin mwa Asia.

Ameeleza kuwa kiasi cha wanawake na watoto milioni nane hupoteza maisha kila mwaka kwa matatizo yanayozuilika. Kati ya hao, milioni mbili ni wahindi. Akizungumza mjini Mumbai katika halfa ya uainzishwaji mkakati wa kuwapiga jeki wanawake na watoto, Ban amesema kuwa takwimu hizo zinamvunja moyo na kumkatisha tama.

Hata hivyo ameweka matumaini yake akisema kuwa mwelekeo huo wa mambo unaweza kurekebishwa.