Hugh Masekela ashiriki kwenye maadhimisho ya muziki wa Jazz duniani

30 Aprili 2012

Mwanamuziki maarufu wa muziki wa Jazz kutoka Afrika Kusini Hugh Masekela alikamilisha matarayisho mwishoni mwa juma pamoja na wanamuziki wengine kwa sherehe za siku ya kimataifa ya Jazz ambayo inaadhimishwa tarehe 30 mwezi Aprili. Siku hii ilianziswa ,mnamo Novemba mwaka uliopita na shirika la elimu , sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO.

UNESCO inasema kuwa ina lengo la kutoa hamasisho kuhusu muziki wa Jazz kama chombo cha kuelimisha na kiungo muhimu cha amani na Umoja kinachochangia kuleta ushirikiano miongoni mwa watu.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud