Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waadhimisha siku ya muziki wa Jazz duniani

UM waadhimisha siku ya muziki wa Jazz duniani

Umoja wa Mataifa unaendelea na sherehe za maadhimisho ya kwanza ya siku ya kimataifa ya muziki wa Jazz kwa tamasha mjini Paris zitakazofuatwa na tamasha zingine kwenye eneo mji wa News Orleans siku ya Jumamosi na kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa siku ya Jumatatu.

Siku ya kimataifa ya Jazz inayoadhimishwa tarehe 30 mwezi Aprili inaangazia mchango ambao umetolewa na muziki wa Jazz katika kuwaunganisha watu na mabadailiko ulioeleta kwenye jamii. Mkurugenzi mkuu wa shirika la UNESCO Irina Bokova amesema kuwa muziki wa Jazz unapita mipaka na kuwaleta watu pamoja. Muziki wa Jazz ulianzia nchini Marekani mwanzo wa karne ya ishirini na hadi sasa una mitindo tofauti kote duniani.