Mataifa ya Afrika yajadili kuanzisha mfuko wa Usalama wa Chakula:FAO

30 Aprili 2012

Uanzishaji wa mfuko wa Afrika kusaidia usalama wa chakula katika bara hilo ni suala lililojadiliwa katika mkutano wa kanda ya Afrika wa shirika la chakula na kilimo FAO uliofanyika Brazzaville Jamhuri ya Congo.

Kwa mujibu wa FAO mfuko huo wa Afrika utachangisha fedha barani humo ili kupambana na njaa na kuruhusu kuongeza mipango itakayozuia na kukabiliana na matatizo ya chakula na kilimo barani humo. Kwa kuunga mkono pendekezo hilo mashirika ya jumuiya za kijamii yaliyohudhuria mkutano huo yalitoa mchango wao kama ishara ya kusaidia mfuko huo.

FAO itajihusisha na mjadiliano yatakayofanyika katika nchi mbalimbali za bara hilo ili kuandika mswaada wa mapendekezo hayo kwa ajili ya kuidhinishwa na nchi wanachama walioshiriki mkutano. Wakati wa mkutano huo Rais wa Jamhuri ya Congo Denis Sassou Ngesso na mkurugenzi wa FAO Jose Graziano da Silva wametoa wito wa mshikamano barani Afrika kusaidia kupambana na matatizo ya usalama wa chakula yanayojitokeza kila mara Sahel na Pembe ya Afrika kwa sasa.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter