Uchaguzi mkuu na serikali iliyo wazi ni muhimu kwa demokrasia:Ban

30 Aprili 2012

 

Uchaguzi na serikali iliyo wazi ni muhimu sana katika kudumisha demokrasia amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon alipohutubia kikao cha bunge nchini Myanmar.

Ameongeza kuwa hata hivyo ni lazima mambo hayo mawili yaambatane na mazingira mazuri ya kisiasa. Katibu Mkuu ameelezea ajenda nne muhimu zitakazolisaidia taifa la Myanmar kusonga mbele katika maridhiano ya kitaifa na kipindi cha mpito cha demokrasia. Miongoni mwa ajenda hizo ni watu wa kawaida lazima waone haraka matunda ya kuelekea demokrasia kila sik katika maish yao, na Myanmar inahitaji ongezeko la misaada ya kimataifa ya maendeleo na uwekezaji wa moja kwa moja.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud