Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza Kuu lafanya tamasha kuadhimisha siku ya kimataifa ya Jazz

Baraza Kuu lafanya tamasha kuadhimisha siku ya kimataifa ya Jazz

Wanamuziki wa Jazz kutoka sehemu mbalimbali duniani watatumbuiza kwenye ukumbi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa katika kuadhimisha siku ya kwanza ya kimataifa ya muziki wa Jazz inayoadhuimishwa Jumatatu Aprili 30.

Wanamuziki hao ni pamoja na mkongwe wa kupuliza trumpet Hugh Masekela na mpiga saxaphon wa Kimarekani Jimm Heath, Angelique Kidjo na wanajazz wapya kama Esperanza Spalding. George Duke ni mshindi wa tuzo ya muziki, mpiga piano, mtayarishaji na muongozaji wa muziki.

(SAUTI YA GEORGE DUKE)

Siku ya kimataifa ya muziki wa Jazz ni mpango uliobuniwa na mpiga piano mkongwe na maarufu duniani Harbie Hancock, na siku ya Jazz ikapitishwa na shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni UNESCO mwezi Novemba mwaka 2011. Tamasha la New York linafuatia lile lililofanyika kwenye mkao makuu ya UNESCO Paris Ijumaa na lile la New Oleans ambako ndio chimbuko la muziki wa Jazz mapema asubuhi ya April 30.