Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ataka suala la maendeleo kuangaliwa upya

Ban ataka suala la maendeleo kuangaliwa upya

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa jamii ya kimataifa inahitaji kutafuta mbinu mpya kuhusu maendeleo. Aliyasema hayo alipokabidhiwa shahada kwenye chuo cha Jamia Millia Islamia nchini India ambapo amesema kuwa kuimarika kwa uchumi hakutoshi.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Ban amesema kuwa zaidi ya akina mama 1000 hufa kila wiki kutokana na matatizo ya uzazi huku mtoto mmoja akifa kila baada ya sekunde ishirini kutokana na maradhi yanayoweza kutibiwa.