Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa UNAIDS aenda Nigeria kuweka msukumo wa kuzuia maambukizi mapya

Mkuu wa UNAIDS aenda Nigeria kuweka msukumo wa kuzuia maambukizi mapya

Mkuu wa shirika la umoja wa mataifa linalojihusisha na ukimwi UNAIDs Michel Sidibé,ameanza ziara ya siku mbili nchini Nigeria ambako anatazamiwa kuweka kipaumbele kwenye maeneo ya kukabiliaana na maambukizi ya virusi vya HIV.

Ziara hiyo inakuja katika kipindi cha mwaka mmoja tangu viongozi wa dunia akiwemo rais Goodluck Jonathan kuzindua mpango wa kimataifa wenye shabaha ya kupusha maambukizi mapya ya HIV kwa watoto wanaozaliwa.

Inakadiriwa kwamba kila mwaka watoto 400 000 duniani kote huzaliwa wakiwa na maambukizi ya virusi vya HIV. Nigeria inatajwa kuwa miongoni mwa nchi zinazokabiliwa na tatizo hilo.