Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM watenga mafungu ya fedha kuwalipa walalamikaji kutokana na uvamizi wa Iraq nchini Kuwait

UM watenga mafungu ya fedha kuwalipa walalamikaji kutokana na uvamizi wa Iraq nchini Kuwait

Kamishana ya Umoja wa Mataifa juu ya ulipaji fidia ambayo ilifanikisha kutanzua mzozo wa fidia kufuatia uvamizi uliofanywa na Iraq nchini Kuwaita imetangaza kutenga kiasi cha dola bilioni 1.2 kwa walalamikaji wa uvamizi huo.

Kiasi hicho cha fedha kilichotengwa kwa walalamika sita walifaulu kukidhi vigezo vyote, kinafanya kamishna hiyo kutumia dola bilioni 36.4 tangu ianze kushughulikia malalamiko ya watu na mataifa mbalimbali.

Kamishna hiyo iliyoanzishwa mwaka 1991kama kitendo kinachofanya kazi chini ya baraza la usalama. Tangu kuanzishwa kwake hadi sasa imepokea jumla ya malalamiko milioni 3 ikiwemo 100 yaliyoletwa na mamlaka za kiserikali.