Ban aipongeza India kwa kuweka msukumo wa pekee kwenye sekta ya afya

27 Aprili 2012

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon aliyeko ziarana nchini India ameipongeza nchi hiyo namna ilivyofaulu kwenye maeneo ya afya lakini hata hivyo ameitaka kuongeza kasi zaidi kuboresha ustawi wa wanawake na watoto.

Katika mkutano wake na waziri wa afya na ustawi wa kijamii Ghulam Nazi Azad Ban alikariri shabaha inayochukuliwa na taifa hilo kuboresha sekta ya afya kwa kuwafaidia raia wote.

Akiwa mjini New Delhi, Ban amekutana na Katibu Mkuu wa chama cha msalaba mwekundi cha India Satya Paul Agarwal na amekipongeza chama hicho namna kinavyochukua mkondo wa juu kushughulikia masuala ya usamaria mwema.

Mwishoni mwa ziara yake anatazamia kutembelea vituo vya afya ambako atashuhudia shughuli mbalimbali zinazofanywa na jamii.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud