Jimbo la Connecticut latupilia mbali hukumu ya kifo

27 Aprili 2012

 

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imekaribisha kutiwa sahihi kwa sheria kwenye jimbo la Connecticut nchini Marekani ambayo inapiga marufuku hukumu ya kifo. Jimbo la California linatarijiwa kuchukua hatua kama hiyo mwezi Novemba huku majimbo mengine nayo yakiombwa kuchukua hatua kama hizo.

OHCHR inatoa ushauri kwa majimbo mengine kupiga hatua ya kuondoa hukumu kali kwenye sheria zao. Kwa sasa mjimbo 17 nchini Marekani yametuma rufaa ya kutaka kutupiliwa mbali hukumu zinazotajwa kuwa kali.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud