Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makambi walioko wakimbizi kutoka Somalia sasa yanakumbwa na mafuriko

Makambi walioko wakimbizi kutoka Somalia sasa yanakumbwa na mafuriko

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa idadi ya wakimbizi wa kisomali kwenye kambi ya Dollo Ado iliyo kusini mwa Ethiopia imefikia wakimbizi 150,000. Kambi hiyo inawapokea takriban wakimbizi 450 kila wiki.

UNHCR inasema kuwa kwa sasa kambi za wakimbizi zilizo nchini Kenya na Ethiopia zinazidi kukumbwa na kiasi kikubwa cha mvua ambazo zimesabbaisha mafuriko na kuharibika kwa barabara. Adrian Edwards kutoka UNHCR anasena kuwa shughuli za usafirisha misaada kwenda kambini zimekwama kufutia mvua hizo.

(SAUTI YA ADRIAN EDWARDS)