Uhuru wa mahakama uko hatarini nchini Papua New Guinea:Pillay

27 Aprili 2012

Serikali ya Papua New Guinea imetakiwa kukoma kubuni sheria ambazo zinakandamiza uhuru wa mahakama. Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay amesema kuwa kubuniwa kwa kipengee ambacho kitawahukumu majaji ni kinyume na sheria akiongeza kuwa hatua hiyo inainyima mahakama uhuru wake.

Pillay amesema kuwa hatua kama hizo zitaleta misukusuko kwenye taiafa hilo, Rupert Colville kutoka ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa anasema kuwa hatua za kuvuruga mahaka nchini Papua New Guinea zimejiri baada ya mzozo kuhusu ni nani kiongozi.

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud