Nchi nyingi masikini hazijapa suluhu ya malaria

26 Aprili 2012

Wakati ulimwengu umeadhimisha siku ya Malaria bado nchi hasa zilizo maskini hazijapata suluhu kamili na njia mwafaka za kupambana na kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa Malaria.

Bado watu wengi hawana uwezo au hawajapata hamasisho kuhusu njia kamili za kujikinga kutokana na ugonjwa wa Malaria ugonjwa ambao husababisha vifo vingi zaidi kwenye nchi hizi.

Ukosefu wa madawa ya kutibu ugonjwa wa malaria na neti za kujikinga dhidi ya mbu pamoja na madawa ya kutibu neti hizo ni baadhi ya masuala yanayoyatia hatarini maisha ya watu wengi kila siku.

Joseph Nzioki ni daktari na mmiliki wa zahanati moja mjini Nairobi nchini Kenya na amezungumza na mwandishi wetu wa Nairobi Jason Nyakundi akizungumzia hali ya sasa ya ugonjwa wa malaria nchini Kenya na jitihada zinazofanywa kukabiliana na ugonjwa huo.

(MAHOJIANO NA DR NZIOKI)