Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maafisa watatu wakongwe wachaguliwa kushika nafasi za juu:UM

Maafisa watatu wakongwe wachaguliwa kushika nafasi za juu:UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewachaguwa wafanyakazi watatu wakongwe wa Umoja wa Mataifa kujaza nafasi za ngazi ya juu zinazohusiana na utawala, msaada wa shughuli za mipango ya nje ya Umoja wa Mataifa na kuangalia huduma za ndani za Umoja huo.

Yukio Takasu kutoka Japan ambaye hivi sasa ni mshari maalumu wa Katibu Mkuu kuhusu usalama wa watu amechaguliwa kuwa msaidizi wa Katibu Mkuu katika upande wa utawala. Takasu ana uzoefu wa takribani miaka 40 katika mambo ya diplomasia. George Njogopa na taarifa zaidi yaw engine waliochaguliwa.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)