Leo ni siku ya wasichana kuwa katika teknolojia ya habari na mawasiliano:ICT

26 Aprili 2012

Leo ni siku maalumu ya wasichana kuwa katika teknolojia ya habari na mawasiliano yaani ICT. Lengo la siku hii inayofanyika hapa mako makuu ya Umoja wa Mataifa New York ni kuwawezesha wasichana kupitia teknolojia ya habari na mawasiliano na kuangalia ni jinsi gani ya kuwachagiza wasichana katika nchi zote duniani kchukua jukumu kubwa katika mapinduzi ya teknolojia.

Siku hii imeandaliwa na muungano wa kimataifa wa teknolojia ya habari ITU ambapo pia umezindua kampeni mpya ya kimataifa iitwayo ”teknolojia inahitaji wasichana” Katika uzinduzi huo wanawake mbalimbali wanaojihusisha na mambo ya teknolojia ya habari na mawasiliano wamealikwa na wanajadilia na kubadilishana mawazo. Miongoni mwao ni Juiana Rotich kutoka Kenya aliyeanzisha mtandao uitwao “Ushahidi” kufuatilia ghasia za machafuko ya baada ya uchaguzi mkuu Kenya 2007.

(SAUTI JULIANA TORICH)

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter