Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mfanya kazi wa kujitolea wa Msalaba Mwekundu auawa Syria:ICRC

Mfanya kazi wa kujitolea wa Msalaba Mwekundu auawa Syria:ICRC

Shirikisho la chama cha msalabla mwekundu katika ulimwengu wa Kiarabu limesema mfanyakazi mmoja wa kujitolea wa chama cha mwezi mwekundu ameuawa na wengine watatu kujeruhiwa wakiwa kazini usiku wa Aprili 24.

Mfanyakazi huyo Mohammed al-Khadraa alikuwa ni mfanyakazi wa huduma ya kwanza kwenye mji wa Doma kwenye vinga vya Damascus na alipigwa risasi na kuuawa akiwa katika gari lililokuwa na nembo ya chama cha msalaba mwekundu.

Chama cha msalaba mwekundu katika nchi za Kiarabu na kamati ya kimataifa ya chama cha msalaba mwekuundu ICRC wamelaani vikali tukio hilo la kutoheshimu wahudumu wanaookoa maisha ya watu nchini Syria.

Kamatio hiyo imesema hayo ni mauaji ya tatu yanayohusisha chama cha msalaba mwekundu katika kipindi cha miezi minane. Wametoa wito wa wahudumu wa afya, vito vya aya, na magari ya wagonjwa kutokashambuliwa kwani wana jukumu kubwa la kuokoa maisha.