Jeshi la DR Congo na MONUSCO wamejitahidi kupunguza nguvu za FDLR:Meece

26 Aprili 2012

Taarifa kutoka Radio washirika wetu Maendeleo ya mjini Bukavu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo zinasema mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini humo Roger Meece, amesema operesheni za jeshi la Congo kwa ushirikiano na mpango wa Umoja wa Mataifa MONUSCO zimepnguza kwa kiwango kikubwa nguvu za kundi la waasi wa Rwanda la FDLR jimboni Kivu ya Kusini Mashariki mwa nchi hiyo.

Meece amesema waasi wengi wa kundi hilo sasa wamerejea Rwanda, hata hivyo amekiri kwamba bado wapiganaji wa kundi hilo ambalo limegoma kuweka silaha chini ni hatari kubwa kwa usalama wa raia. Ameahidi kwamba MONSCO itaendelea kulisaidia jeshi la Congo katika kuhakikisha usalama wa raia.

(SAUTI YA ROGER MEECE)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud