Leo ni miaka 26 tangu kutokea zahma ya nyuklia ya Chernobyl

26 Aprili 2012

Leo Alhamisi ni miaka 26 tangu kutokea kwa zahma ya nyuklia ya Chernobyl, ajali ambayo ilikuwa mbaya zaidi ya nyuklia kuwahi kutokea katika historia.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon katika kumbukumbu hii amesema dunia inawakumbuka mamia ya wafanyakazi wa huduma za dharura ambao walihatarisha maisha yao kusaidia wengine waliokumbwa na ajali ambapo watu 330,000 waliondolewa kwenye eneo la tukio wakiwa na matumaini madogo saana ya kurejea.

Amesema maelfu ya watoto walipatwa na saratani ya tezi na watu wengine milioni sita bado wanaishi katika maeneo yaliyoathirika ya Belarus, shirikisho la Urusi na Ukraine.

Ban amesema pamoja na kuyakumbuka yaliyopita ni lazima kutazama mbele amesema Umoja wa Mataifa umejidhatiti kuendelea ksuaidia katika ujenzi mpya na maendeleo ya eneo hilo, kwa lengo la kuzisaidia jamii husika kuabiliana na mazingira wanayoishi. Mwaka jana Ban alizuru Chernobyl na kujionea mwenye ari waliyonayo watu walioathirika katika kuganga yajayo.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter