Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi wanachama waafikiana kuhusu jukumu la UNCTAD katika miake minne ijayo

Nchi wanachama waafikiana kuhusu jukumu la UNCTAD katika miake minne ijayo

 

 Kongamano la 13 la mkutano wa Umoja wa Mataifa wa biashara na maendeleo limemalizika Alhamisi Doha Qatar kwa kuafikiana kuupitisha mkataba wa Doha. Mkataba huo unaelezea jukumu la UNCTAD katika kipindi cha miaka mine ijayo eneo ambalo lilizusha mjadala mkubwa wa jinsi gani ya kukabiliana na matatizo ya fedha kwa kuzingatia kazi za UNCTAD na ilikuwa vigumu hadi saa ya mwisho ambapo wamekubaliana kwamba UNCTAD itaangalia tuu suala la athari za mgogoro wa fedha katika nchi zinazoendelea na sio chanzo chake. Taffere Tasfachew ni msemaji wa kongamano hilo la 13.

(SAuTI YA TAFFERE TASFACHEW

Wakati wa mjadala huo nchi zinazoendelea zimeelezea kwamba kujikwamua kutoka katika matatizo ya uchumi hakujakamilika na baadhi ya wajumbe walihisi kwamba chombo hicho cha moja wa mataifa kingeruhusiwa kuchambua chanzo sio tuu athari. Katika miaka minne ijayo UNCTAD itasaidia nchi zinazoendelea na hususani zile masikini kabisa na ambazo uchumi wake uko katika kipindi cha mpito.