Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi wanachama wametakiwa kuridhia mkataba wa uhalifu wa UM

Nchi wanachama wametakiwa kuridhia mkataba wa uhalifu wa UM

Nchi wanachama wametakiwa kuridhia na kutekeleza mikataba ya Umoja wa Mataifa ya kupambana na uhalifu na ufisadi. Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon wakati Baraza la Usalama lilipokuwa likijadili amani na usalama wa kimataifa Jumatano.

Katibu Mkuu amesema mashirika ya kikanda ni muhimu katika kushughulikia mitiririko na usafirishaji haramu wa watu. Ban amesema kuna haja ya kuwa na mifumo ambayo itang’amua na kufuatilia kile alichokiita uingizaji mkubwa wa fedha haramu zinazopatikana kutokana na shughuli za kihalifu katika nchi mbalimbali.

Ameongeza kuwa Umoja wa Mataifa unazisaidia nchi zinazotetereka na zisisojiweza zikiwemo zile ambazo zinachipukia kutoka kwenye vita ili kuweza kulinda mipaka yake.