Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban asumbuliwa na hatua ya Israel ya ujenzi wa makao

Ban asumbuliwa na hatua ya Israel ya ujenzi wa makao

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa anasumbuliwa na uamuzi wa Israel wa kuidhinisha ujenzi wa makao kwenye eneo la ukingo wa magharibi akiitaja hatua hiyo kuwa haramu chini ya sheria ya kimataifa.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na msemaji wake Ban amesema kuwa shughuli zozote za ujenzi zinaenda kimyume na mpango wa amani ambao unazitaka pande husika kujizuia na vitendo vya uchokozi. Mapema mwezi huu kundi na pande nne ukiwemo Umoja wa Mataifa, muungano wa Ulaya, Urusi na Marekani wameishauri Israel na Palestina kujizuia na vitendo vinavtoleta kutoaminiana kati yao ukiwemo ujenzi wa makao mapya.