Wanawake zaidi wanatakiwa kwenye mabaraza ya maamuzi

25 Aprili 2012

Baraza la Usalama limepewa shime kuunga mkono juhudi zinazotaka kuongezeka kwa idadi ya wanawake kwenye mabaraza ya maamuzi

Kwa mujibu wa afisa mtendaji kitengo cha masuala ya wanawake kwenye Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet amesema kuwa uchaguzi ndiyo fursa pekee ambayo itawawezesha wanawake wengi kuingia kwenye ofisi za umma na pia kuibua mijadala ya kisera inayohusu usawa kwa wanawake.

Amesema kuwa katika chaguzi tano za mabunge zilizofanyika mwaka 2011 ambazo wajumbe wa Umoja wa Mataifa walishuhudia,kumekuwa na ongezeko kiasi kwa wanawake kwenye chaguzi hizo. Matokeo mengi kwenye chaguzi hizo amesema kuliwa na wastani wa asilimia 10 ya viti vya ubunge vilivyoangukia mikononi mwa wanawake.

Baraza la Usalama lilikutana siku ya jumanne kujadilia masuala mbalimbali ikiwemo wanawake, amani na usalama.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud