Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lalaani vikali mashambulizi kwa vikosi vya kulinda amani vilivyoko Darfur

Baraza la Usalama lalaani vikali mashambulizi kwa vikosi vya kulinda amani vilivyoko Darfur

Baraza la Usalama kwa kauli moja limelaani vikali matukio ya kushambuliwa kwa vikosi vya ulinzi wa amani katika eneo la magharibi wa jimbo la Darfur nchini Sudan , ambako maafisa wane walijeruhiwa na mmoja kati yake anasadikika kufariki dunia kutokana na majeraha makubwa.

Kundi hilo la askari polisi likiwa kwenye doria ya kawaida kwenye eneo hilo, lilivamiwa na watu wenye silaha na kushambuliwa na kuwajeruhi askari kadhaa. Pamoja na kulaani vikali shambulio hilo, Baraza la Usalama limetuma salama za rambi rambi kwa vikosi vya askari hao pamoja na familia zao.

Limeitaka serikali ya Sudan kuendesha uchunguzi wa haraka ili kuwabaini wahusika wa tukio hilo na hatimaye kuwafikisha kwenye mkono wa sheria.