Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Asia inahitaji nishati safi kukuza uchumi:ESCAP

Asia inahitaji nishati safi kukuza uchumi:ESCAP

Kuleta uwiano wa maendeleo endelevu na kiwango kikubwa cha ukuaji wa uchumi kunahitaji makubaliano ya nishati mpya kwa mataifa ya Asia na Pacific amesema afisa wa Umoja wa Mataifa anayehusika na mataifa hayo kwenye kongamano la watunga sera lililofanyika Jumatano.

Afisa huyo Noeleen Heyzer ambaye ni Katibu Mkuu wa tume ya Umoja wa Mataifa ya uchumi na jamii kwa nchi za Asia na Pacific ESCAP amesema uchumi wa Asia Pacific ni chachu ya ukuaji lakini ili kufanya uendelee unahitaji nishati safi, endelevu na inayopatikana kwa urahisi.

Ameongeza kuwa mataifa hayo yanahitaji nishati itakayoleta mabadiliko ili kuhakikisha kwamba kila mmoja anapata nishati hiyo muhimu, kupunguza hali tegemezi ya mafuta, kuboresha matumizi ya nishati na kuongeza mara mbili matumizi ya nishati mbadala Asia na Pacific ifikapo 2030.