Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi wanachama wanapunguza tofauti za jukumu la Shirika la UM la Biashara

Nchi wanachama wanapunguza tofauti za jukumu la Shirika la UM la Biashara

Nchi wanachama bado hawajaafikiana kuhusu jukumu la shirika la Umoja wa Mataifa la biashara na maendeleo kwa miaka mine ijayo, lakini wanafanya juhudi kupunguza tofauti zao.

Huu ni ujumbe uliotyolewa na Taffere Tesfachew msemaji wa muktano wa Umoja wa Mataifa wa biashara na maendeleo unaofanyika Doha Qatar. Amesema hatua zimepigwa kuhusu endapo matokeo ya mkutano wa Doha yasisitize mkataba wa Accra ambao uliweka jukumu la UNCTAD kwa miaka minne iliyopita.

Nchi wanachama pia wamefikia makubaliano ya endapo UNCTAD iendelee kufanya kazi katika Nyanja ya fedha suala nyeti baina ya nchi zilizoendelea na zinazoendelea. Hata hivyo amesisitiza kwamba baadhi ya tofati bado zipo.

(SAUTI YA TAFFERE TESFACHEW)

Kongamano hilo la kimataifa la UNCTAD limepangwa kumalizika Alhamisi April 26.