Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ushirikiano wa biashara wa Kusini-Kusini ni muhimu:UNCTAD

Ushirikiano wa biashara wa Kusini-Kusini ni muhimu:UNCTAD

Mawaziri na maafisa kutoka pande zilioridhia maafikiano ya mfumo wa kimataifa wa kutoa kipaumbele katika masuala ya biashara miongoni mwa nchi zinazoendelea GSTP wamerejea kuonyesha nia yao ya kuyaleta matokeo ya Sao Palo katika utekelezaji kwa kusistiza mipango ya nchi kuridhia.

Wajumbe hao ambao wametoa taarifa maalumu kwenye kongamano la 13 la kimataifa la biashara UNCTAD huko Doha Qatar wamesema ingawa kupitia ushirikiano huo wataanzisha masharti ya lazima kwa ajili ya kukuza uchumi wao na hasa kufaidika na ushirikiano wa biashara na Kusini-Kusini. Wamesema wanashawishika kwamba kwa kuongeza msukumo kwa ushirikiano wa Kusini-Kusini itachangia ukuaji wa biashara duniani na kunufaisha uchumi wa dunia kwa ujumla.