Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Malaria bado ni tishio kubwa la maisha wa watu duniani:WHO

Malaria bado ni tishio kubwa la maisha wa watu duniani:WHO

Malaria bado inawakilisha matatizo makubwa ya afya duniani huku nchi 99 zikiendelea kukabiliwa na maambukizi ya ugonjwa huo na watu zaidi ya 650,000 wakifariki dunia kila mwaka kutokana na ugonjwa wa Malaria.

Shirika la Afya Duniani WHO katika kuadhimisha siku ya Malaria Duniani ambayo kila mwaka huwa Aprili 25 linazindua mkakati mpya ujulikanao kama T-3 ambazo ni Test yaani pima, Treat yaani Tibu na Track yaani Fuatilia. Tarik Jasarevic kutoka WHO anafafanua kuhusu umuhimu wa mradi huo.

(SAUTI YA TARIK JASAREVIC)

Kwa mujibu wa WHO vifo vya Malaria duniani vimepungua kwa zaidi ya robo tangu mwaka 2000. Karibu nusu ya nchi zinazozongwa na Malaria zimepunguza vifo kwa zaidi ya asilimia 50 kati ya mwaka 2000 na 2010. Hii ni kutokana na usambazaji na matumizi ya vyandarua vyenye dawa, na watu wengi zaidi kupata dawa za kudhibiti ugonjwa huo.