Serikali ya Syria yatakiwa kushirikiana na waangalizi

24 Aprili 2012

Serikali ya Syria imeshauriwa kutoa ushirikiano na waangalizi wa kimataifa waliotumwa kukagua usitishwaji wa ghasia kwenye taifa hilo. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewaambia waandishi wa habari kuwa anashirikiana na mjumbe maalum wa nchi za kiarabu na Umoja wa Mataifa Kofi Annan wakati kunapoendelea na mipango ya kutuma waangalizi 300 wa Umoja wa Mataifa nchini Syria.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliamrisha kutumwa kwa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Syria ambao utafahamika kama UNSMIS.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud