WHO yasema itaisaidia Vietnam kukabiliana na ugonjwa usiotambuliwa

24 Aprili 2012

Visa vya ugonjwa usiojulikana vimeripotiwa kwenye mkoa wa Quang Ngai nchini Vietnam. Wanaougua ugonjwa huo wanatoka kwenye kijiji cha Ba Dien na wanalalimikia kuumwa kwa tumbo na mara nyingi ugonjwa huo husaabisha kuharibika kwa ini. Tangu Aprili mwaka 2011 ugonjwa huo umesabaisha vifo vya watu wanane na kusababisha kuugua kwa watu wengine 171. Dalili za ugonjwa huo zilitoweka mwezi Oktoba mwaka uliopita na kuonekana baadaye mwezi Machi mwaka huu.

Wizara ya afya nchini Vietnam pamoja na vituo vinavyohusika na utafiti wa magonjwa fwamekuwa wakiendesha utafiti wa kwanza ulioanza mwaka 2011 huku wa pili ukiandaliwa Aprili 13 mwaka huu. WHO inasema kuwa iko tayari kuisaidia Vietnam kukabilina na ugonjwa huo usiojulikana.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter