ICC kufuatilia uwezekano wa uhalifu wa vita Mali

24 Aprili 2012

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC imesema inafuatilia kwa karibu hali nchini Mali na itachunguza kwa kina endapo uhalifu wa vita, uhalifu dhidi ya ubinadamu au mauji ya kimbari vimetekelezwa nchini humo.

Katika taarifa yake iliyotolewa Jumanne ofisi ya mwendesha mashitaka wa ICC imesema ina ripoti kutoka vyanzo mbalimbali ikiwemo kutoka maafisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa za kuhusu mauaji, utekaji, ubakaji na uingizaji wa watoto jeshini unaofanywa na makundi mbalimbali Kaskazini mwa Mali.

Ofisi ya mwendesha mashitaka imesema itaamua wakati muafaka endapo ianzishe uchunguzi. Askari waasi walitwaa madaraka Machi 22 baada ya kufanbya mapinduzi ya kijeshi, wakimshutumu rais aliyeondolewa madarakani Amadou Toumani Toure kwa kushindwa kuwawezesha wanajeshi wa serikali kukabiliana na waasi wa Tuareg Kaskazini mwa nchi.

Waasi wa Ruareg wamelitangaza eneo la Kaskanini kuwa huru lakini tangazo hilo limepingwa vikali na nchi jirani na Muungano wa Afrika. Na baada ya ECOWAS kuweka vikwazo kufuatia mapinduzi sasa wanamapinduzi hao wamekubali kuunda seriikali ya mpito ili kuandaa uchguzi mpya.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud