Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kawi itachangia katika kuangamiza umasikini:Supachai

Kawi itachangia katika kuangamiza umasikini:Supachai

Katibu Mkuu kwenye shirika la biashara na maendeleo la Umoja wa Mataifa UNCTAD Supachai Panitchpakdi amesema kuwa umaskini hautaangaziwa bila kuwepo kwa kawi. Ameelezea umuhimu unaochangiwa na kawi katika ukuaji wa uchumi. Amesema kuwa matumizi ya gesi yananastahili kuinuliwa kwenye nchi zinazoendelea kwa kuwa inachangia katika kupunguza uchafusi wa hewa ni moja ya njia za kuyahakikishia kawi mataifa maskini siku za usoni. Suala hilo lilijadiliwa kwenye mkutano maalumu kuhusu matumizi ya gesi uliondaliwa na shirika la UNCTAD.