Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ugonjwa wa Surua waripotiwa barani Afrika, Ulaya na Asia

Ugonjwa wa Surua waripotiwa barani Afrika, Ulaya na Asia

Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa kumeripotiwa mkurupuko wa ugonjwa wa Surua kote duniani huku asilimia kubwa ikiripotiwa barani Afrika, Ulaya na Asia. WHO inasema kuwa chanjo iliyotolewa kati ya mwaka 2000 na 2010 imechangia kupunguza vifo vinavyosababishawa na ugonjwa wa surua kwa asilimia 85.

WHO kwa ushirikiano na shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF pamoja na washirika wanajaribu kuhakikisha kuwa vita dhidi ya ugonjwa surua vimeendelea. Dr Peter Strebel ni kutoka shirika la WHO.

(SAUTI YA PETER STREBEL)