Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yakamilisha kusambaza huduma za dharura kwa wakimbizi wa Syria walioko Iraq

IOM yakamilisha kusambaza huduma za dharura kwa wakimbizi wa Syria walioko Iraq

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM limekamilisha zoezi lake la usambazaji wa misaada ya chakula kwa wakimbizi wa Syria walioko katika kambi ya Dahuk iliyoko katika eneo linalotawaliwa na Wakurdistan kaskazini mwa Iraq.

Pamoja na misaada ya hiyo ya chakula IOM pia imesambaza huduma nyingine kadhaa, ikiwemo vifaa vya kuchuja maji, mablanketi, vifaa vya kupikia.

Kwa upande wake shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR limekamilisha pia kusambaza huduma nyingine kama vifaa vya jikoni, mafuta ya taa na vifaa vingine.

Zoezi hilo limefanya kwa mashirikiano ya mashirika hayo mawili, ikiwa ni mara ya tatu sasa katika kipindi cha wiki tatu zilizopita.