Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM yakaribisha enzi mpya ya upashaji wa habari kwa mifumo ya digitali

UM yakaribisha enzi mpya ya upashaji wa habari kwa mifumo ya digitali

Umoja wa Mataifa umesema kuwa unachukua mkondo mpya wa upashaji habari zake, lakini wakati huo huo utaendelea kutegemea pia njia zake za zamani za utoaji taarifa kupitia vyombo kama radio,luninga na magazeti kuwasilisha taarifa zake.

Afisa wa ngazi za juu wa Umoja huo Maher Nasser amesema kuwa kukua na kupanuka kwa sekta ya wamasiliano ambayo inashuhudiwa mabadiliko ya mara kwa mara, ni hatua ambayo Umoja wa Mataifa unapaswa kwenda sambamba nayo.

Kaimu huyo wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa amesema kuwa hatua ya Umoja wa Mataifa kuhamia kwenye mfumo wa digitali ni uamuzi uliofanywa kwa kuzingatia mahitajio halisi ya wakati wa sasa na yanakwenda kulingana na mabadiliko ya teknolojia.

Pamoja na kukaribisha enzi mpya digitali, lakini amesisitiza kwamba Umoja wa Mataifa utaendelea kutumia mifumo yake ya awali ya upashaji habari, mifumo ambayo ameeleza kuwa bado inaheshimika na inafanya kazi kwa ufanisi mkubwa.