Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban kufanya ziara nchini Myanmar

Ban kufanya ziara nchini Myanmar

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon anatarajiwa kufanya ziara nchini Myanmar mwishoni mwa juma ambapo atakutana na viongozi wa nchi hiyo wakati taifa hilo linapoingia kwenye kipindi cha mabadiliko.

Ban ameyasema hayo baada ya kukutana na kundi lijulikanalo kama marafiki wa Myanmar kundi la nchi 14 pamoja na muungano wa Ulaya. Ban amesema kuwa kumeshuhudiwa mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi kwenye taifa hilo kwa muda wa mwaka mmoja uliopita ukiwemo uchagzui wa hivi majuzi. Ban ameongeza kuwa akiwa nchini Myanmar atampongeza rais Thein Sein pamoja na kiongozi wa upinzani Aung San Suu Kyi ambaye alijishindia kiti cha ubunge hivi majuzi.