Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi wa Syria kupokea misaada ya chakula

Wakimbizi wa Syria kupokea misaada ya chakula

Karibu raia 250 wa Syria wanatarajiwa kupokea misaada ya chakula kutoka kwa shirika la mpango wa chakula duniani WFP. Kwa ushirikiano na chama cha mwezi mwekundu nchini Syria WFP itatoa misaada kwenye miji ya Homs, Hama, Idleb na Damascus.

WFP inasema kuwa ina mipango ya kuongeza maradufu idadi ya wale inaowapa chakula miezi inayokuja. Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa karibu watu milioni moja wanahitaji misaada ndani mwa Syria baada ya machafuko ya kisiasa kuikumba nchi hiyo. Elisabeth Byrs ni kutoka WFP.

CLIP