Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNDP, AFP zakubali kushirikiana kukabili changamoto za kimaendeleo

UNDP, AFP zakubali kushirikiana kukabili changamoto za kimaendeleo

Shirika la Maendeleo ya Umoja wa Mataifa UNDP limetiliana saini ya mashirikiano na shirika la maendeleo la Ufaransa AFD, kwa shabaha ya pande zote mbili kufanya kazi kwa karibu zaidi ili kuharakisha mipango ya kimaendeleo hasa wakati huu kuelekea kwenye mwaka wa malengo ya maendeleo ya milenia.

Pande zote mbili zimekubaliana kuongeza mashirikiano ili kusukuma mbele kasi ya ufikiaji wa lengo la kutokomeza umaskini. Kwa pamoja, mashirika hayo yanakusudia kuanzisha mipango itayosaidia kuzikabili changamoto zinazokwamisha kutofikia malengo hayo ya melenia.

Yamekubaliana kuongeza juhudi ili kuzikwamua changamoto za mabadiliko ya tabia nchi, tatizo la ajira kwa vijana na kusuma mbele dhana ya mashirikiano baina ya mashirika ya umma na yale ya kibinasfi.